
MSANII wa filamu mwenye matukio ya kusisimua bongo, Rehema Fabian, amenusulika kufa baada ya kunywa dawa inayodaiwa kuwa ni sumu ya mende kwa kile alichodai kuwa amechoka kuandamwa na watu.
Tukio la kunywa dawa hiyo kwa msanii huyo lilitokea wiki iliyopita ambapo mwandishi wa habari hizi alishuhudia msanii huyo akiwa katika hali ngumu ingawa alikunywa maziwa na kutapika sumu yote.
Akizungumzia ishu hiyo rafiki wa karibu na msanii huyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kuwa Fabian hakuwahi kutaka kujiua lakini alishangazwa pale alipochukua dawa hizo na kuzinywa huku akijua fika kuwa ni sumu ya mende.
Chanzo hicho kilisema baada ya kunywa dawa hizo alindondoka chini mara tatu, na ndipo walipowahi kumpa maziwa kitu ambacho kilimsaidia kutapika sumu yote.
“Yenye mwenyewe anadai kuwa amechoka kuandamwa na watu lakini kauli hiyo hata sisi rafiki zake imetuweka njia panda kwani hatuelewi chochote,” kilisema chanzo hicho. Hata hivyo Rehema mwenyewe alidai kuwa kuna wimbi la watu limekuwa likimfatilia kila kitu anachokifanya lakini hajui nini kinachosababisha tatizo hilo.
“Jamani nashindwa kuelewa ni kwanini kila napofanya kitu lazima watu watoa taarifa zangu kwa wazazi wangu, kweli nachukia tabia hii, najua lengo lao ni kutaka nionekane mbaya mbele ya wazazi wangu,” alisema.
Source : DarTalk.com
