Kwenye hali yakibaridiridi baada ya mvuwa nyingi iliyo piga kwenye ukumbi wa Musee Vivant ambayo ilikuwa ni sehemu pekee iliyo kuwa imeandaliwa kwa tamasha hiyo kabambi ambayo ilikuwa imeingiya kwenye mwaka wake wa 2,kwani mwaka wa kwanza ilitangazwa rasmi kupitiya Radio bila kukusanya watu nakuwatambulisha mshindi kupitiya tamasha.Hiyo imefanyika baada ya sapoti ya hali ya juu ambayo iliyo onekana kwa makampuni makubwa makubwa nje na ndani ya Burundi,tukizungumziya kampuni kabambi inayo peperusha nakuzitangaza kazi za wanasanaa tofauti wa miziki na sinema.Kampuni ya GLM inayo ongozwa na PASTEUR BAGENZINIKINDI mrundi anae ishi USA ila iko karibu sana na nchi yake,kampuni hiyo imejitoleya ku utangaza muziki kupitiya Internet imeimarika vyema kuwa imesaidiya kwa hili ao lile ili tamasha hiyo ifahanikishe,apo tusisahau Kampuni ya vinywaji Brarudi ambayo ilijitoleya jukwa lakisasa ambayo imejizatiti vyuma vyote muhimu ili tamasha ifanyike.Kwa ujumla tamasha haikuendeka walivyo kuwa wanavyo fikiriya walio anda mashindano hayo kwani kasoro kubwa zilijitokeza,kwanza tatizo la ufundi apo tukizungumziya umeme ambao ulikuja kuwa sugu nakusababisha hata mashabiki kunungunika.Kwenye ratiba ilikuwa wanamuziki wote walio chaguliwa kufika kwenye atuwa ya fainali kuimba ila hawakuimba,tamasha hiyo ilianza inakawiya kwanza kutokana na mvuwa kali iliyo vamiya mji mkuu Bujumbura na tayizo hilo nililo simuliya hapo juu.Wageni tofauti wa vituo vya Radio,makampuni na wapenzi bila kusahau wadadisi na wakongwe kwenye game la mziki huu apa walijumuika kwa pamoja ili ku ipa shavu competition hiyi.Mnamo kama saa mbili ya usiku na nusu(20h30)ndipo walipo tangazwa washindi kwenye mashindano hayo.Mkurugenzi wa Radio Isanganiro akishindikizwa na RALLYE-Joe ndio waliyo funguwa kwa ujumbe mfupi walio utowa ili kuonyesha mshikamano wano kwa jumuiya ya watu walio itika wito huyo.Mr Happy,Exellent NIMUBONA na Christian Nsavye walikuwa tayari kwa kuwapasha waliyo udhuriya gisi mambo yalivyo kuwa yanakwenda na ndio walio anza kuwa ita kwenye jukwa wakianziya kwenye namba ya 10 hadi ya 1.Fahamu ya kwamba kati yanyimbo zilizo wakilishwa kwenye hatuwa ya fainali,waliyo zi imba apo nazungumzia THE COUSINS hawakuwepo walikuwa kwenye tamasha mkowani Gitega ambapo walikuwa walikwenda kutambulisha kwa mara nyingi album yao ‘The Cousins in the game’,habari zilizo tufikiya ni kwamba tamasha hiyo ilikwenda vizuri,alitwambiya DJ Ashanti Wapekee tulipo muarifu kwa sim akiwa jijini pale.
Walishindano ifwatavyo:
10.LUGHA ZETU by THE COUSINS 90 points
9.YAMBOGORERA by EMELANCE EMY 102 points
8.NIKOZUBAKWA by RIZIKI 162 points
7.NDABARAMUTSA by T MAX 188 points
6.SHEBA by R FLOW 298 points
5.NI NDE! by PEACE & LOVE 304 points
4.ISHURE by MKOMBOZI 493 points
3.UTUNYONI/WIBAZA NGO! by LION STORY 667 points
2.IMBABAZI by LION STORY 681 points
1.WIYUMVA GUTE? by YOYA 1002 points
YOYA ambae ni mzaliwa baada ya mashindano mawili ya TEN IN ONE na yale yakuadimisha miaka 2 ya SMART kufanyika nakuto shinda sasa yuko mbinguni(Il est aux Anges),ivo basi kinyume nakupewa tunzo nzuri atafanyiwa bonge la promotion na Radio Isanganiro mwaka mzima kwa vipindi flani watakavyo kuwa wanamfanyiya ili kumtambulisha nje na ndani ya BURUNDI,nyimbo WIYUMVA GUTE? imepiku na fasi REKA NTAHE ya RALLYE-Joe ambayo ilisaliya kwenye na fasi ya 1 mwaka mzima kwenye Radio hiyo.Pongezi kwa ISSA DJAMAL…
Read Also



