‘RESPECT NYERERE’ KUZINDULIWA SERENA HOTEL APRIL 14 – STEVE NYERERE…!!

By glmteam
Posted on 05 Feb 2012 at 7:25am

Source : Dartalk.com

MSANII wa filamu za kisiasa bongo na Afrika Mashariki, Steve Nyerere, amesema kuwa kazi yake ya‘Respect Nyerere’, imekamilika na inatarajiwa kuzinduliwa kwenye hoteli  ya Serena, Aprili 14 mwaka huu.

Akizungumza na mtandao wa DarTalk, msanii huyu alisema kitu kilichobakia katika filamu hiyo ni kutoa baadhi ya vipande ambavyo havitakiwi ili iweze kwenda sokoni ikiwa na maadili halisi ya Kitanzania.

Alisema filamu hiyo inaweza kuchukua sura mpya katika siasa kwani imeeleza matukio makubwa ambayo yanaichafua nchi kwa sasa huku baadhi ya viongozi wakichuma mali na kuacha watanzania wakiwa maskini.

Steve akiwa kwenye maandalizi ya filamu hiyo

“Filamu imekamilika na itazinduliwa Aprili 14, hivyo nawaomba mashabiki wa filamu zangu wakae tayari kuziona kwani kuna matukio mengi ya kusisimua ambayo yatakuwa na mafunzo makubwa ndani ya jamii yetu,” alisema.

Hata hivyo nyota huyo aliongeza kuwa malengo yake ni kucheza filamu za zenye matukio halisi na ambayo yanaweza kutokea hapo baadaye endapo jamii au Serikali haitabadilika katika baadhi ya mambo ambayo Watanzania wamekuwa wakiyalalamikia.

 


Read Also