
MSANII ambaye ni mama wa watoto watatu Thea, amesema kuwa mchakato wa kuanza kutoa filamu zake umekamilika na sasa anaipeleka sokoni kazi yake ya ‘Zawadi ya Christmas’.
Alisema kazi hiyo amecheza kwa kiwango cha hali ya juu, ingawa msanii huyu hakueleza ni namna gani alivyotumia ubunifu ili kuwavutia mashabiki wake.
“Filamu hiyo ni zawadi kwa mashabiki, najua inaweza kuwa na mapungufu kwani mimi nilicheza humo ni binadamu hivyo siwezi kufanya mambo yote yakawa mazuri, ingawa naamini nimefanya mambo mazuri ambayo yatakuwa na mvuto kwa mashabiki wangu,” alisema Thea.
Sambamba na ujio wa filamu hiyo, aliongeza kuwa anafanya kazi kwa lengo kujitoa katika wimbi la umaskini, pia ni jukumu lake kuwaelimisha watanzania kwa sababu ni msanii na kioo cha jamii.
Read Also
