MSANII mkongwe katika tasnia ya filamu bongo, Aunty Fifii, baada ya kufanya vizuri na kazi ya ‘Kizungumkuti’, aliyoitoa mwaka jana, sasa anakamilisha nyingine mpya inayokwenda kwa jina la‘Queen Spear’.
Ndani ya filamu hiyo kutakuwa na wasanii kama Hemed Suleiman ‘PHD’, Mzee Chilo, Mama Kawele, wengine ni Jackline Pantezel, Pastor Nyamba, Mama Sonia, Shija na Pacho Mwamba.
Akizungumza na DarTalk, msanii huyo alisema kuwa filamu hiyo kwa sasa ipo katika hatua za mwisho kukamilika na inaweza kuwa sokoni baada ya wiki tatu hadi nne. Alisema kuwa uzinduzi wa filamu hiyo utafanyika katika nchi mbalimbali za Afrika kama ilivyokuwa ya ‘Kizungumkuti’, ambayo ilizinduliwa nchini Burundi.

